Wasiom-post Esma wapewa dongo

HomeBurudani

Wasiom-post Esma wapewa dongo

Mfanyabiashara Esma Platnumz ambaye ni dada wa msanii na mmiliki wa lebo ya Wasafi Diamond Platnumz amewachana wale ambao hawakumtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa ilhali yeye huwaweka kwenye ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa anashukuru kama waliona kwa kufanya hivyo ingechafua kurasa zao.

Asante kwa wote mlioniwish Birthday yangu ktk page zenu Mungu awabariki Mwaka huu uwe wa mafanikio, Na wale wasioniwish birthday kuogopa mtachafua page zenu ila mi niliwawish ktk page yangu niwatakie kila lenye heri mwaka huu wa 2022 inshallah ,Mungu atubariki kwa Sote,” ameandika Esma.

Kaka yake Esma, Diamond alimtakia heri dada yake huyo kwa kuchapisha picha yake kwenye ukurasa wake wa instagram huku akimwambia yupo nje ya nchi lakini akirudi atamletea zawadi yake aliyomuandalia na kuwakumbusha mashabiki kufika siku ya tarehe 14 mwezi wa pili kwa ajili ya shughuli waliyoianda siku hiyo ya wapendanao.

“a very special day to my Beloved sister Esma Platnumz… Nimeshindwa kukupa zawadi yako ya Birthday leo….ila bado iko pale pale, tarehe 14 Mlimani City ntakupatia..Love you sis tena Mahaba Ndindindi,” ameandika Diamond. 

error: Content is protected !!