Vipaumbele vya Zuhura Yunus baada ya uteuzi

HomeKitaifa

Vipaumbele vya Zuhura Yunus baada ya uteuzi

Aliyewahi kuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Zuhura Yunus ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ametaja vipaumbele vyake kuwa ni kukuza mawasiliano ya taasisi hiyo ya Ikulu, wizara, serikali na waandishi wa habari.

“Pale (Ikulu) ilikuwa kupata watu kuzungumza na sisi (waandishi wa habari) ilikuwa ni mtihani na wakati mwingine unakuta labda taarifa wanazo lakini hawajui jinsi gani ya kuzitoa. Jambo kubwa ni kuweka muungano mzuri baina ya Rais Samia Ikulu na wizara zake na waandishi wa habari wa ndani na wa kimataifa ili kuwe na hali nzuri ya kuwasiliana,” alisema Zuhura.

Alizungumza hayo katika mahojiano maalumu baina yake na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC)  na kusema ana uhakika ataimudu nafasi hiyo na kwamba jambo muhimu ni kuweka mfumo mzuri wa mawasiliano.

Rais Samia Suluhu alimteua Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Jaffar Haniu ambaye atapangiwa kazi nyingine kwa mujibu wa taarifa zilizotoka.

 

error: Content is protected !!