IGP Wambura aanza kazi

HomeKitaifa

IGP Wambura aanza kazi

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camilus Wambura amewataka wananchi wa jiji la Arusha kuendelea kutunza amani iliyopo na kutokujiingiza kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani hasa kipindi hiki ambapo kuna mkutano mkubwa wa Marais kutoka nchi saba za afrika mashariki.

IGP Wambura amesema hayo baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Polisi mkoa wa Arusha na kupokelewa na kamanda wa Polisi mkoani humo Justin Masejo ambapo aliwataka askari kuendelea kusimamia amani na kuwachukulia hatua kali wale wote watakaobainika kutaka kuvuruga amani ya nchi.

IGP Wambura pia ameahidi  kushughulika na yeyote ambaye atakuwa na vitendo vyovyote kinyume na maadili na kinyume na matendo mema ya Watanzania. 

 

error: Content is protected !!