Msemaji wa kisekta wa ACT-WAZALENDO, Dorothy Semu, amesema hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, bungeni kuhusu suala la mfumuko wa bei za bidhaa halikupewa uzito kwa kuwa walitarajia kuona inatoa suluhu ya tatizo la kiuchumi, jamii na siasa linalolikabili taifa kwa sasa.
“Unawezaje kutoa mabilioni ya fedha kununua ndege katika mazingira ambayo wananchi hawawezi kukabili bei ya sukari, mafuta ya kula, mchele, Maharagwe na ngano? ACT-Wazalendo inaelekeza kwa serikali kuwa ni lazima ifunge mikanda kwa matumizi yake na itoe nafuu kwa jamii kwa kupunguza kodi zake angalau Sh.500 kwa kila lita moja ya mafuta ya dizeli ili kuwahami wananchi,” alisema Dorothy.
Mbali na hayo, Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema serikali itapunguza kodi kwa bidhaa zinazoingia nchini ili kumpunguzia mwananchi mzigo wa kupanda bei ikiwa ni agizo la Rais Samia Suluhu kuchukua hatua za muda mfupi za kukabiliana na tatizo hilo.