Afa maji akikimbia polisi

HomeKitaifa

Afa maji akikimbia polisi

Hassani Mussa M’buyu (27) mkazi wa mtaa wa Sabasaba, Kata ya Jamhuri, Manispaa ya Lindi amekufa maji, baada ya kujitosa baharini kwa madai ya kukimbia kukamatwa na polisi kwa tuhuma za kutishia kumuua mpenzi wake.

ACP Mtatiro a,ethibitisha tukio hilo na ksuema M’buyu ambaye alikuwa ni mwendesha bodaboda, alichukua uamuzi huo, Aprili 4 mwaka huu saa 12:30 jioni.

“Huyu M’buyu baada ya kufika kituoni pale alielekezwa aende chumba cha dawati la jinsia,” alisema ACP Mtatiro.

Kamanda  alisema baada ya mlalamikiwa kufika mlango wa chumba cha dawati, alimkuta mpenzi wake akiwa ndani ameshawasili na kuamua kuchukua hatua ya kukimbia, askari walimkimbiza lakini alikataa kusimama na kujitosa baharini na kufariki.

Sharifa Zakaria (23) ambaye ni mlalamikaji alisema yeye na M’buyu walikuwa wapenzi na kubahatika kubeba ujauzito lakini hakuwa anampatia huduma yotote hata alipolazwa hospitalini akisumbuliwa na maumivu ya tumbo hakuwahi kwenda kumuona kumjulia hali.

 

error: Content is protected !!