AfDB yaipatia Tanzania mkopo wa bilioni 175.5 kwa ajili ya wakulima

HomeKitaifa

AfDB yaipatia Tanzania mkopo wa bilioni 175.5 kwa ajili ya wakulima

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), imeipatia Tanzania mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Marekani milioni 75 (Sh. bilioni 175.5) kusaidia upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakulima.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba, alisema Mei 31 mwaka huu, Tanzania iliiomba AfDB kufadhili utafiti na kuendeleza uzalishaji wa mbegu na utoaji wa mbolea.

“ Leo (jana) ndani ya siku zisizozidi 90, tunashuhudia utiaji saini wa mradi huu muhimu kwenye jamii yetu na uchumi kwa ujumla. Kwa kuzingatia hayo, sina budi kuipongeza AfDB kuwa mshirika wa maendeleo wa karibu katika nchi yetu hata katika nyakati ngumu tunazopitia,” alisema Tutuba.

Alisema fedha hizo ni sehemu ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP- III) na sehemu ya ajenfa ya serikali inayolenga kujenga uchumi shindani wa viwanda kwa maendeleo ya watu kwa kuboresha miundombinu kwenye sekta za uzalishaji.

Alisema pia ni sehemu ya upatikanaji wa nishati endelevu, kuimarisha mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji wa pamoja na mifumo ya elimu na mafunzo.

error: Content is protected !!