Abiria 41 waliokuwa wakisafiri na basi la Happy Nation wakitokea Dar es Salaam kuelekea Mwanza, wamenusurika katika ajali baada ya basi lao kugongana uso kwa uso na lori aina ya Scania katika eneo la Mkambarani, mkoani Morogoro.
Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Morogoro, ACP Ralph Meela, ameeleza kuwa chanzo cha ajali ya basi la Happy Nation lililogongana uso kwa uso na lori aina ya Scania katika eneo la Mkambarani, mkoani Morogoro ni uzembe wa dereva wa basi hilo aliyeacha njia yake na kulifuata lori.
Katika ajali hiyo, dereva wa basi hilo la Happy Nation amejeruhiwa na ameshapelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi huku abiria wote wakiwa salama.