Amuua baba yake baada ya kumkuta amelala na mkewe

HomeKitaifa

Amuua baba yake baada ya kumkuta amelala na mkewe

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga , linamshikilia Mwandu Shija (32) mkazi wa Ndala Manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi, Shija Robert (55) kwa madai ya kumfumania akiwa amelala na mke wake kitandani.

George Kyando, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 8:00 usiku wakati kijana huyo aliporudi nyumbani na kumkuta baba yake akiwa maelala na mke wake ndipo alipoanza kumshambulia.

Kamanda Kyando alisema wakati kijana huyo akiendelea kumshambulia baba yake na kipande cha kuni sehemu mbalimbali za mwili wake, ndipo alipompiga sehemu mbaya na kusababisha mauaji.

“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi, baada ya marehemu kukutwa akiwa amelala na kitanda kimoja na mke wa mtuhumiwa.

“Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari na kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ukisubiri kukabidhiwa kwa wanandugu kwa ajili ya maziko,” alisema Kamanda Kyando.

 

SOURCE: NIPASHE

error: Content is protected !!