Askofu Shoo: Michango ya Rais Samia kwenye makanisa na misikiti sio rushwa

HomeKitaifa

Askofu Shoo: Michango ya Rais Samia kwenye makanisa na misikiti sio rushwa

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo nchini Tanzania CCT, Askofu Dkt. Fredrick Shoo amesema Rais Samia Suluhu anapotoa michango kwenye makanisa na misikiti isitafsiriwe kama ni hongo. Askofu Shoo amesema, Rais Samia anafanya hivyo kwa unyenyekevu na hofu yake kwa Mungu.

Askofu Mkuu Shoo amesema hayo July 03, 2025 Jijini Dodoma wakati wa Mkutano Mkuu wa 32 wa CCT ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo.

“Baadhi yetu tulivyotafsiri na walivyotafsiri vibaya pale ambapo Rais kama Rais lakini kama Mtu mwenye hofu ya Mungu na anaheshimu sana Dini, anavyotoa michango kwa kazi mbalimbali za Kanisa na za Misikiti, kipekee imeniumiza pale ilipotafsiriwa kwamba hii ni hongo”

“Mahali pengine tunahitaji hekima, tunahitaji uelewa mzuri, tusifanye tu kama kuna sababu ya kumpinga Rais kwa namna yoyote ile, kumchukia kwasababu zako mwenyewe, kwa hiyo naomba Rais kwa unyenyekevu wake na kwa hofu yake anapotoa mchango kwa kazi ya kuwahudumia Watu wa Mungu naomba sana tukwepe makosa makubwa ya kumsingizia kitu ambacho hajadhamiria kwenye moyo wake kwamba hii sasa ni rushwa”

Aidha, Askofu Shoo amesema anamuomba Rais Samia aendelee kuwa mvumilivu, asikate tamaa na pia aendelee kuunga mkono kazi za Mungu.

error: Content is protected !!