Aunty Ezekiel amkaanga Ruby

HomeBurudaniUncategorized

Aunty Ezekiel amkaanga Ruby

 

Mwigizaji wa filamu kutoka nchini Tanzania, Aunty Ezekiel ambaye pia ni mke wa msanii Kusah, amesema kwamba aliyewahi kuwa mchumba wa mume wake nyota wa kike wa muziki Ruby, anajua kuimba na ni msanii mzuri ila tu hana riziki hivyo apambane atafute pesa.

“Sijapost lakini ni nina mpango wakumpostia nyimbo yake pia ili ziweze kwenda, sio msanii mbaya anajua kuimba ila hana riziki, kwahiyo ninatakiwa kumsukuma afike kule anakotaka kufika au afike kule ambako kutampa riziki, kwa sababu mwisho wa siku hakaika, zunguka lakini pesa ndio kila kitu, kwahiyo acha ujeuri tafuta hela,” alisema Aunty.

Aliongea hayo akiwa anajibu swali la mwandishi wa habari kuhusu kinachoendelea kati ya wawili hao kwa sababu hivi karibu kwenye mitandao ya kijamii hasa instagram Aunty na Ruby wameonekana wakirushiana maneno njia ya mafumbo.

Ikumbukwe kwa sasa Aunty amezaa mtoto mmoja wa kiume na Kusah ambaye hapo awali alishakuwa na mtoto wa kike na msanii Ruby kabla ya wawili hao kutengana na Ruby kuanzisha mahusiano na aliyewahi kuwa mchumba wa Aunty Ezekieli, Mose Iyobo.

error: Content is protected !!