Bei ya umeme kwa uniti

HomeKitaifa

Bei ya umeme kwa uniti

Waziri wa Nishati, January Makamba ametangaza Sh.1,600 kuwa bei mpya ya umeme kwa uniti, katika maeneo yanayopata huduma hiyo nje ya gridi, hasa umemejua.

Ametoa tangazo hilo katika ziara yake wilayani Ukerewe, Kisiwa cha Ukara ndani ya Ziwa Victoria mkoani hapa, akasema bei hiyo itaanza kutumika Agosti mosi mwaka huu, baada ya kutangazwa rasmi kwenye gazeti la serikali na mamlaka husika.

“Bei hii si hapa tu Ukara, bali kwa maeneo yote nchini yanayopata nishati hiyo nje ya gridi,” amesistiza.

Gharama hiyo imepanda kutoka Sh.100 kwa uniti wanayolipa wananchi kwa takribani miaka miwili, baada ya kushushwa kutoka Sh.3,500 kwa uniti.

Amesema kushushwa hadi Sh.100 kumemfanya muwekezaji, ambaye ni Kampuni ya Jumeme kushindwa kumudu gharama za uzalishaji, hivyo kulazimika kutoa huduma hiyo kwa mgao, kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni tu.

 

error: Content is protected !!