Boss Shell, apongeza maboresho mazingira ya uwekezaji Tanzania

HomeKitaifa

Boss Shell, apongeza maboresho mazingira ya uwekezaji Tanzania

‘Rais Samia Suluhu Hassan amezungumza kwa njia ya mtandao na Ben Van Beurden, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Royal Dutch Shell yenye makao yake makuu nchini Uholanzi.

Van Beurden amemshukuru Rais Samia na kueleza kuwa wanaridhishwa na jinsi Serikali ya Awamu ya Sita ilivyoboresha mazungumzo ya uwekezaji  kwenye mradi wa Gesi asili iliyosindikwa (LNG) hapa nchini.

Kwa upande wake Rais Samia amemshukuru Van Beurden kwa nia yao njema ya kutaka kuwekeza kwenye mradi huo ambao utachochea kukuza uchumi wa Tanzania.

  > Maagizo ya Serikali kwa mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania

Kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao Ikulu Chamwino mkoani Dodoma, kimehudhuriwa na Waziri wa Nishati, January Makamba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi. Leonard Masanja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio.

error: Content is protected !!