Mahakama nchini Korea Kusini imemkuta na hatia ‘Boss’ wa Samsung, Jay Lee aliyekuwa askishtakiwa kwa makosa ya kutumia dawa ambazo zimekatazwa kutumika na binadamu wasio na matatizo yanayohitaji kutibiwa kwa dawa hizo.
Dawa hizo ambazo hutumika kuondoa au kupunguza maumivu kwa watu wanaofanyiwa upasuaji zimepigwa marufuku kwa mujibu wa sheria za Korea Kusini na zimewekewa mipaka zitumike kwa minajili ya matibabu, na sivinginevyo.
Watu wa kawaida huweza kuzitumia dawa hizo kupata usingizi, kupunguza msongo au kupunguza maumivu, ambapo ni kinyume na sheria ikiwa agizo la matumizi halikutoka kwa Daktari.
‘Boss’ huyo wa Samsung ambaye amekutwa na hatia ya kutumia dawa mara 14 kati ya mwaka 2015 na 2020, ameiambia Mahakama kuwa anajuta kufanya hivyo.
Wafanyakazi wa Hospitali waliompa Lee dawa hiyo bila kufuata utaratibu wamefunguliwa mashtaka tofauti.Kesi hii itamfanya atozwe faini ya takribani milioni 120 na fidia nyinginezo huku hukumu kamili ikitarajiwa kutoka Oktoba 26.