Baada ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kumaliza kulifungua rasmi na kulihutubia Bunge leo Novemba 14, 2025 jijini Dodoma, shughuli za Bunge zimehitimishwa kwa hatua ya kuliahirisha hadi mwakani.
Katika hatua hiyo Spika wa Bunge Mussa Zungu alimuita Waziri Mkuu Dk. Mwigulu Nchemba, ambaye alitoa salamu za shukrani kwa Rais, Wabunge na kwa Spika mwenyewe na kisha kuomba Bunge kumuunga mkono hoja ya kuahirisha shughuli za Bunge hadi Januari 27, 2026.
Hoja hiyo iliungwa mkono na Wabunge na kupitishwa rasmi na Spika, hivyo kuhitimisha mkutano huo wa Bunge la Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Bunge litarejea Januari 27, 2026 kuendelea na majukumu yake ya kutunga sheria, kusimamia Serikali na kuwakilisha wananchi.


