Mwenye asili ya Scotland ateuliwa kuongoza jeshi Zambia

HomeKimataifa

Mwenye asili ya Scotland ateuliwa kuongoza jeshi Zambia

Rais (mpya) wa Zambia, Hakainde Hichilema ameteua wakuu wapya wa kamandi za jeshi na kuwabadilisha makamishna wote wa polisi ikiwa ni mkakati wa kusuka upya idara ya ulinzi na usalama nchini humo.

Alitoa uamuzi huo jana lakini licha ya kwamba hakueleza sababu, uamuzi huo umetajwa kuwa ni mkakati wake wa kukomesha ubabe wa majeshi ya nchi hiyo, ambao aliushuhudia mara kadhaa alipokamatwa wakati akifanya shughuli zake za kisiasa chini ya uongozi wa Rais Edgar Lungu.

Miongoni mwa teuzi hizo, uteuzi wa Kamanda wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Zambia kimeibua sintofahamu mitandaoni. Sintofahamu hiyo imetokana na aliyeteuliwa, Luteni Jenerali Collins Barry kuwa na asili ya Scotland.

Barry ni mtoto wa baba kutoka nchi hiyo ya Ulaya ambaye alikuwa akifanya kazi kama mwalimu wa kujitolea katika Shule ya Ufundi ya Solwezi nchini Zambia, na mama yake ni raia wa Zambia.

Luteni Barry amesoma shule nchini Zambia na alipata mafunzo ya urubani katika Jeshi la Anga la Zambia.

Rais Hichilema amewataka polisi kufuata sheria na kuagiza mtuhumiwa yeyote asikamatwe hadi hapo upelelezi wa tuhuma zake utakapokamilika.

error: Content is protected !!