Kipindi anachorekodi Rais Samia Suluhu

HomeKitaifa

Kipindi anachorekodi Rais Samia Suluhu

Taarifa iliyotolewa na Ikulu leo Agosti 29 2021, inaeleza kwamba Rais Samia Suluhu ameanza kurekodi kipindi maarufu cha ‘Royal Tour’ kwa lengo la kuitangaza Tanzania.

Royal Tour ni nini?
Mwanahabari Peter  Greenberg kutoka Marekani, amekuwa akitembelea nchi mbalimbali na kutengeneza kipindi chenye lengo la kutangaza nchi hizo. Katika nchi hizo, viongozi wakuu walimtembeza katika vivutio mbalimbali.Amewahi kufanya hivyo katika nchi kama New Zealand akiwa na Helen Clark aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Israel akiwa na  Benjamin Netanyahu aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mexico akiwa na Felipe Calderon aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, na Rwanda akiongozwa na Rais  Paul Kagame.

Maudhui hayo huwekwa katika kipindi cha ‘Royal Tour’ kinachorushwa na kituo cha PBS huko Marekani na kutazamwa na mamilioni ya watu kupitia mtandao.

Hapa Tanzania, Rais Samia Suluhu atamuongoza Peter Greenberg kurekodi kipindi hicho katika maeneo mbalimbali ya Tanzania ili kuweza kutangaza vivutio vilivyopo.

error: Content is protected !!