Historia ya Yanga na mgogoro uliopeleka Simba kuanzishwa

HomeMichezo

Historia ya Yanga na mgogoro uliopeleka Simba kuanzishwa

 

kuanzishwaHistoria ya Klabu ya Yanga inatokea tangu enzi za miaka ya 1910, ingawaje historia kamili ilianza kuandikwa mwaka 1935. Klabu hiyo ilitokana na desturi ya vijana wa Dar es salaam waliokuwa wakikutana viwanja vya jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda wakaamua kuunda timu yao iliyojulikana kwa jina la Jangwani Boys.

Ndani ya kipindi kifupi timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo, miongoni mwao waliovutiwa na uanachama wa klabu hiyo ni Tabu Mangala (Sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926 walifanya mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi sasa kuna shule ya sekondari ya Tambaza. Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wafanyakazi wa bandari na mashabiki wake wengi walikuwa wabeba mizigo bandarini. Baada ya mkutano huo, timu ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za Waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika. Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa wana wa Jangwani hao.

Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama na washabiki wa timu hiyo walikuwa wanatembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani wao, kwamba katika kipindi hicho wao ndiyo zaidi. Kwasababu Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka wakati huo, wanachama wa timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Italiana. Italiana FC ilipata mafanikio ya haraka na haikushangaza ilipopanda ligi daraja la pili kanda ya Dar es Salaam.

Mwanzoni mwa miaka ya 1930 Italiana waliamua kuachana na jina lao mapema kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo wakaanza kujiita New Youngs. Kila ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu vipya pia, kwani wakiwa na jina la New Youngs waliweza kutwaa Kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam.

Mwaka 1935 uwezo wa Klabu ulishuka sana kusababisha wanachama kutofautiana na kuleta migogoro katika Klabu na ulisababisha baadhi ya wanachama kujiengua na kuanzisha Klabu nyingine. Wanachama walioasi Klabu waliunda Klabu iliyojulikana kwa jina la Queens F.C. ambayoa baadaye ilibadilisha jina na kuitwa Sunderland ambayo kwa sasa inajuliakana kama Simba S.C.

Baada ya mgawanyiko wanachama waliobaki waliifanyia marekebisho klabu yaliyopelekea kubadilisha jina kutoka New Youngs to Young Africans. Washabiki wengi walishindwa kutamka jina la Young kwa ufasaha ambao ilipelekea kuzaliwa kwa jina la “Yanga”.

Yanga kama timu ya wananchi ilileta hamasa sana katika nchi na kusaidia kuunganisha wananchi kipindi cha kupigania uhuru wa nchi. Yanga imekuwa na mafanikio makubwa sana tangu kuanzishwa kwake. Ikiwa na miaka Zaidi ya 85 imekuwa na mafanikio yafuatayo;

1. Washindi wa Ligi Kuu ya Tanzania mara 27- 1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1987, 1991, 1996, 1997, 2000, 2005, 2006, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13, 2014–15, 2015–16, 2016–17.

2. Washindi wa Kombe la Tanzania mara 4 – 1975, 1994, 1999, 2015–16

3. CECAFA Club Cup/Kagame Interclub Cup mara 5 – 1975, 1993, 1999, 2011, 2012.

4. Kombe la Mabingwa la CAF – Imeshiriki mara 11
1997 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)
1998 – Hatua ya Makundi (Group stage)
2001 – Hatua ya Pili (Second Round)
2006 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)
2007 – Hatua ya Pili (Second Round)
2009 – Hatua ya Kwanza (First Round)
2010 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)
2012 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)
2014 – Hatua ya Kwanza (First Round)
2016 – Hatua ya Pili (Second Round)
2017 –

5. Kombe la Klabu Bingwa Africa – Imeshiriki mara 11
1969 – Robo Finali (Quarter-finals)
1970 – Robo Finali (Quarter-finals)
1971 – Ilijitoa Hatua ya Pili (withdrew in Second Round)
1972 – Hauta ya Kwanza (First Round)
1973 – Hatua ya Kwanza (First Round)
1975 – Hatua ya Pili (Second Round)
1982 – Hatua ya Pili (Second Round)
1984 – Hatua ya Kwanza (First Round)
1988 – Hatua ya Kwanza (First Round)
1992 – Hatua ya Kwanza (First Round)
1996 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)

6. Kombe la Shirikisho la CAF: Imeshiriki mara 4
2007 – Hatua ya Kati (Intermediate Round)
2008 – Hatua ya Kwanza (First Round)
2011 – Hatua ya Mwanzo (Preliminary Round)
2016 – Hatua ya Makundi (Group stage)
2018 – Hatua ya Makundi (Group stage)

7. Kombe la CAF: Imeshiriki mara 2
1994 – Hatua ya Kwanza (First Round)
1999 – Hatua ya Kwanza (First Round)

8. CAF Cup Winners’ Cup: Imeshiriki mara 2
1995 – Hatua ya Robo Finalia (Quarter-finals)
2000 – Hatua ya Kwanza (First Round)

error: Content is protected !!