Bunge lapiga kura ya kutokuwa na imani ya Rais

HomeKimataifa

Bunge lapiga kura ya kutokuwa na imani ya Rais

 

Bunge la Taifa la Chile limepiga kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Rais wa nchi hiyo Sebastian Pinera baada ya tuhuma za kuvunja sheria za mauzo kwa kuuza mgodi nchini humo bila kufuata utaratibu. Kura za awali imeshapigwa na kupitishwa na wabunge na sasa hatua inayofuata ni kwenye upande wa seneti.

Baada ya mdahalo wa takribani saa 22 Bungeni, wabunge walipiga kura, na kura 78 zikapigwa kuonesha kutokuwa na imani ya Rais huyo, huku 67 zikimuunga mkono. Baada ya utaratibu huo hatua inayofuata ni Maseneti 43 ambao watapiga kura, itahitajika theluthi 2 za kura zote za maseneta kumng’oa madarakani Rais huyo.

Tukio la kumng’a Rais huyo madarakani limekuja baada ya taarifa za Pandora kutoka na kuonesha kuwa Rais Pinera anahusika kwenye mitandao ya fedha haramu duniani na vigogo wengi kutoka sehemu mbalimbali za Dunia. Moja ya nyaraka hizo ni nyaraka inayoonesha kuwa 2010 Rais Pinera aliuza mgodi wa Dominga, mgodi wa chuma na shaba nchini Chile. Mwaka 2010 Rais Pinera alikuwa na mwaka mmoja madarakani, na amekanusha vikali tuhuma zinazomkabili.

error: Content is protected !!