CCM: Siasa zitumike kutuunganisha

HomeKitaifa

CCM: Siasa zitumike kutuunganisha

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema siasa zitumike kuunganisha watu, zilete upendo na umoja na wazikatae siasa za chuki na wanasiasa wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kwa kutumia matukio mbalimbali kuchochea migogoro na kuvuruga umoja uliopo.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM), Kenani Kihongosi ameeleza hayo Mei 17,2026 alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya CCM kata ya Kabarimi Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Akizungumza katika mkutano huo Kihongosi amesema siasa zinapaswa kuunganisha wananchi, kuleta upendo na kuimarisha umoja badala ya kutumiwa kama njia ya kugawa jamii.

“Siasa zituunganishe, siasa zilete upendo, siasa zilete umoja msije na haya mambo, lazima tuambizane. Kataeni siasa za hovyo na wanasiasa wanaotafuta umaarufu wa kisiasa,” amesema.

error: Content is protected !!