CHADEMA yawasilisha hoja 6 Mahakama Kuu

HomeKitaifa

CHADEMA yawasilisha hoja 6 Mahakama Kuu

Baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kuamua wabunge 19 wa CHADEMA waliovuliwa uanachama kuendelea kuwapo bungeni hadi maombi ya zuio la muda yatakaposikilizwa Juni 13, mwaka huu na kutolewa uamuzi, Mawakili wa chama hicho, Peter Kibatala na Jeremia Mtobesya wamewasilisha hoja sita za kupinga ombi la kuondolewa amri hiyo kutokana na upungufu katika maombi na viapo vya waleta maombi.

Kibatala alidai kuwa katika hoja ya kwanza viapo vya waleta maombi sehemu moja wanesaini mawakili badala ya waleta maombi, pingamizi la pili hakuna kiapo kinachotaja dini zao, hamna kiapo kama dini, uhai wa kiapo ni maombi yenyewe.

Pingamizi la tatu, Kibatala alidai maombi yaliyowasilishwa hayajaonyesha kuwa yanataka nini na dhidi ya kina nani, amri ikitolewa itakuwa imetolewa dhidi ya nani na kwamba haitaeleweka.

“Amri za mahakama zinatakiwa ziwe zinaeleweka na kutekelezeka. Mheshimiwa Jaji haujaombwa, kwa hiyo hawawezi kutoa amri sababu hakuna sehemu waliyopeleka kufikia kutoa nafuu hizo,” alidai Kibatala.

Pingamizi la nne, Kibatala aneleza kuwa amri haiwezi kutolewa kwa sababu Bunge (Katibu wa Bunge) hayupo katika shauri hilo, wakati ofisi yao ndiyp inashughulikia masuala ya waleta maombi.

Wakili Kibatala anaendelea luwasilisha mapingamizi yake, kuwa katika pingamizi la tano Katiba inakataza suala lililofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchunguzwa.

Pingamizi la sita, hakuna sababu zozote zilizotolewa kuonyesha kwamba kuna hatari itatokea kama waleta maombi wakitolewa bungeni.

Halima Mdee na wenzake wamewasilisha maombi mawili Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ya kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama na Baraza Kuu la CHADEMA ambalo lilikaa Mei 12,2022 na kufikia uamizi huo baada ya kupigwa kura nyingi.

error: Content is protected !!