Waziri angongwa na bodaboda

HomeKimataifa

Waziri angongwa na bodaboda

Ofisa wa ngazi ya juu katika Serikali na chama cha upinzani cha Sudan People’s Liberation Movement in Opposition(SPLM-IO), Lual Lual Gau, amejeruhiwa baada ya kugongwa na kuangushwa na bodaboda Kaskazini mwa mji mkuu wa Jimbo la Bahr el Ghazal, Aweil.

Taarifa zinaeleza kwamba Lual alilaumu tukio hilo kwa ofisa mkuu wa seriklai kutembea kwa miguu na kurudi nyumbani kwa miguu katika jimbo hilo.

“Ninatoa mwito kwa serikali kutoa stahili za mawaziri wote kama vile usalama maadamu tu, wanateuliwa katika ngazi ya serikali au kitaifa,

“Sababu kuu ya ajali hiyo nilikuwa natembea kwa miguu. Nilikuwa nikienda kliniki ya Aweli kwa matibabu kabla ya ajali..,nilikuwa nikienda nyumbani kutoka kliniki iliyopo uwanja wa ndege majira ya saa moja jioni. Mita chache kutoka kliniki, mlevi akiwa kwenye pikipiki alikuja kwa kasi na hakuwa na taa kwenye pikipiki yake iliyokuwa na abiria, ghafla nilihisi kugongwa nikaokolewa na watu wa karibu na hospitali,” alieleza.

 

error: Content is protected !!