Fahamu faida za kulala ofisini

HomeKitaifa

Fahamu faida za kulala ofisini

Kulala kwa angalau dakika 30 ukiwa kazini ni kitu muhimu sana kwani mwili umekua umechoka kwa kufanya kazi kwa muda mrefu hivyo unapojipumzisha na kisha kuamka unakuwa na nguvu mpya ya kuendelea.

Faida za kulala ofisini

Kuwa makini zaidi
Unapolala katikati ya siku hasa baada ya kula chakula cha mchana, utakapo amka unakuwa makini na kile ulichokuwa unafanya na kufanya kazi yako kwa ufanisi na umakini.

Kuwa mbunifu
Unapolala kazini na kisha kuamka akili yako inakuwa mpya na hivyo kuwa na uwezo wa kuongeza ubunifu juu ya kile ulichokuwa unafanya.

Kuongeza utunzaji wa kumbukumbu
Unapolala akili nayo inatulia na hivyo kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu kwani ukiwa na mambo mengi bila kupumzika akili nayo inachoka na hivyo kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha.

 

error: Content is protected !!