Ziara ya Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba nchini China imezaa matunda baada ya China kuahidi kushirikiana na Tanzania katika uzalishaji wa nishati jadidifu chini ya mpango wa Belt and Road Energy Partnership.
Kutokana na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya nchi hizi, China imeahidi kutoa fursa za mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalam wa Tanzania katika ubunifu na uzalishaji wa teknolojia za uzalishaji wa nishati na kushirikiana katika utafutaji na uendelezaji wa miradi ya nishati ya gesi asilia jambo linalotiliwa mkazo na Rais Samia Suluhu.
Katika ziara hiyo Waziri Makamba alikagua baadhi ya mitambo ya kufua umeme katika Bwawa la Julius Nyerere inayozalishwa nchini China katika kiwanda cha Kampuni ya Dong Fang Global jijini Sichuan.