Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping wameshuhudia kusainiwa kwa mikataba na hati za makubaliano ya kimkakati 15.
Miongoni mwa mikataba hiyo ililenga kuimarisha ushirikiano, biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo mbili.
Mikataba na hati zilizosainiwa:
- Kuwepo kwa soko la usafirishaji wa maparachichi kutoka Tanzania kwenda China
- Wametia saini mkataba unaohusu msaada wa RMB milioni 100 za ushirkiano wa kiuchumi na kitaalamu
- Makubalino ya kuwepo kwa soko kubwa la usafirishaji wa mabondo ya samaki na bidhaa nyingine za uvuvi kutoka Tanzania kwenda China
- China imetoa mkopo wa thamani ya dola za KImarekani milioni 56.72 wenye masharti nafuu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Zanzibar, Terminal II
Pia, serikali ya China imeipongeza Serikali ya Tanzania kwa mafanikio iliyopata kwenye maendeleo chini ya Rais Samia Suluhu.
Aidha, katika tamko la pamoja, Rais Samia Suluhu na Rais Xi Jinping walikubaliana kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa nchi hizo kutokana na matunda yaliyopatikana katika uhusiano wa miaka 58 iliyopita.