Chuo cha VETA kujengwa Rungwe

HomeKitaifa

Chuo cha VETA kujengwa Rungwe

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameutaka uongozi wa Wilaya ya Rungwe kutafuta eneo la zaidi ya Hekari 20 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa chuo cha ufundi stadi-VETA.

Waziri Mkenda ameyasema hayo jana tarehe 7 Agosti 2022 alipopewa fursa ya kujibu hoja zilizoibuka wakati wa ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan Wilayani Rungwe ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mbeya iliyoanza tarehe 5 Agosti 2022 hadi leo tarehe 8 Agosti 2022.

Waziri Mkenda amesema kuwa Katika bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2022/2023 zimetengwa Bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa Vyuo vya Ufundi stadi-VETA katika wilaya mbalimbali nchini hivyo Wilaya ya Rungwe ni mojawapo katika mpango huo.

error: Content is protected !!