Dar yaongoza kuwa na wagonjwa wa mabusha na matende

HomeKitaifa

Dar yaongoza kuwa na wagonjwa wa mabusha na matende

Utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTDPC) mwaka jana mkoani Dar es Salaam, umebainisha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inaongoza kwa kuwa na maambukizi ya vimelea vya ugonjwa wa mabusha na matende.

Halmashauri hiyo ni sehemu ya halmashauri za wilaya tisa ambazo mpaka sasa kwa mujibu wa utafiti huo ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Mtama mkoani Lindi, bado zina zaidi ya asilimia mbili ya maabukizi ya ugonjwa huo.

Mkoa wa Dar es Salaam kesho unatarajia kufanya uzinduzi wa utoaji wa kingatiba katika manispaa tatu ambazo bado zina maambukizi, Manispaa hizi ni Kinondoni, Temeke na Jiji la Ilala. Kingatiba hiyo itaanza kutolewa Novemba 21 hadi 25 mwaka huu.

error: Content is protected !!