Ed Sheeran kufanya remix ya ‘Peru’ na Fireboy DML

HomeBurudani

Ed Sheeran kufanya remix ya ‘Peru’ na Fireboy DML

Nyota wa muziki kutoka Uingereza, mtunzi wa nyimbo na mwimbaji pamoja na mshindi wa Grammy, Ed Sheeran ameweka wazi nia yake ya kufanya kazi na nyota kutoka nchini Nigeria, Fireboy DML kupitia wimbo wa ‘Peru” unaofanya vizuri sana Afrika na nje kwa ujumla.

Amesema hayo wakati wa mahojiano ya dakika 15 na mwimbaji mashuhuri, mpiga kinanda na mtunzi Elton John kwenye jukwaa la ‘Rocket Hour’, Ed Sheeran alizungumza jinsi ilivyokuwa mpaka akaamua kufanya remix ya wimbo huo na Fireboy.

“Kuna rafiki yangu alinitumia wimbo huo na kuniambia kwamba nyota huyo wa YBNL angependa niwepo kwenye remix ya wimbo wake, lakini Peru ni wimbo ninao upenda na nimekuwa nikusikiliza mara kwa mara,” alisema Ed Sheeran.

Pia Ed Sheeran amesema baada ya kutumiwa wimbo huo akaupenda na tayari ameshatunga mashairi ya kipande chake kitakachokuwa kwenye wimbo huu, ikumbukwe hii sio mara ya kwanza kwa Nyota huyu wa Uingereza kuimba na wasanii kutoka Nigeria kwani tayari ameishaimba na Burna Boy wimbo wa ‘Own It’.

error: Content is protected !!