Exclusive: Rayvany amuangukia Konde Boy

HomeBurudani

Exclusive: Rayvany amuangukia Konde Boy

Nyota kutoka Konde Gang, Harmonize amesema kwamba Rayvanny alishawahi kumpigia simu zaidi ya mara 5 akimtaka asivujishe sauti yake inayosikika akiongea na kumponda bosi wake Diamond Platnumz miaka mitatu iliyopita baada ya mmiliki wa huyo konde Gang kutoka kwenye lebo ya Wasafi.

Harmonize amendika Rayvanny alishawahi kumpigia lakini hakupokea simu zake, hivyo akampigia Jose wa mipango meneja wa Ibrah ili aweze kumuomba asitoa sauti hizo na yeye akaona ni vyema akakaa nazo na kutoziachia. Hata hivyo siku ya jana aliachia sauti hizo kwa waandishi wa habari huku akitaja sababu ni kwamba ameona anatengenezewa mazingira ya kuonekana mmbaya.

“Akawa anamuomba Jose wa Mipango kuongea na mimi nisivujishe voice note kitu ambacho sikuwa nafikiria kwa sababu kila alichosema ni cha kweli, na alikua upande wangu 100%. uzuri Jose wa Mipango alimrekodi mkitaka na hiyo nawapatia pia, baada ya kuona imeshindikana akaona njia pekee ni kujiwahi kufanya na Dissim online na Wasafi , kumbuka nimekaa na hiyo voice note miaka mitatu nimeweka wazi leo baada ya kuona natengenezewa ubaya kia siku,” ameandika Harmonize.

Tangu ameongea maneno hayo na kuachia sauti hizo zinazosikika wawili hao wakiongea mpaka sasa Rayvanny hajasema chochote wala Diamond naye hajatia neno katika hili.

error: Content is protected !!