Facebook yaonya matumizi ya Parody (akaunti feki)

HomeKimataifa

Facebook yaonya matumizi ya Parody (akaunti feki)

Facebook imeiandikia jeshi la polisi la Los Angeles (LAPD) kuacha matumizi ya akaunti fake ambazo wanazitumia kwa ajili ya kuchunguza wahalifu mitandaoni.

Kulingana na sera za matumizi ya mtandao wa Facebook inapinga vikali matumizi ya akaunti feki kwenye mtandao wake. Lengo la Facebook ni kuweka mazingira ya mtandao wake kuwa salama kwa kila mtumiaji, na kila mtu awe na imani na amani kuwa hakuna madhara yatamtokea pindi atumiapo mtandao huo.

Idara ya polisi ya Los Angeles imesema kupitia barua pepe kuwa mtandao wa Facebook umesaidia na unazidi kuwa na manufaa katika kufichua wahalifu mitandaoni, hivyo kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kupunguza uhalifu, madawa ya kulevya na mauwaji.

error: Content is protected !!