Fahamu tuzo 5 maarufu zaidi duniani

HomeElimu

Fahamu tuzo 5 maarufu zaidi duniani

Dunia ina tuzo za kila aina zinazotolewa kwa watu wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali.

Zipo tuzo nyingi zinazofahamika sana duniani, zifuatazo ni baadhi ya tuzo hizo;

1. Tuzo za Nobel 

Tuzo hizo zilizoanzishwa na mwanasayansi wa Swideni, Alfred Nobel zilianza kutolewa mwaka 1901.

Ni tuzo ambayo mshindi anapewa kiasi kikubwa cha fedha na nedali ya dhahabu kama sehemu ya zawadi na hutolewa katika vipengele sita ambavyo ni kemia, fizikia, fasihi, afya, uchumi na amani.

2. Ballon d’OR

Ni tuzo zinazotolewa kwa wanasoka. Kila mwaka, jarida la Ufaransa liitwalo ‘Ballon d’Or’ hutoa tuzo kwa mwanasoka bora wa dunia, katika tukio ambalo hufuatiliwa duniani kote.

3. ‘The Academy Awards’

Zinafahamika zaidi kama tuzo za Oscar ambapo hutolewa kwa wanaofanya vizuri katika uigizaji (filamu).

Tuzo hizo zilizoanzishwa mwaka 1929, hutazamwa na watu zaidi ya bilioni moja ulimwenguni.

4. Tuzo za Grammy

Tuzo hizi hutolewa kwa wanaofanya vizuri kwenye aina za muziki kama ‘jazz’, ‘country’ na iana nyingine.

Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 1959 huko Uingereza.

5. Tuzo za ‘BET’

Ni kati ya tuzo zinazoheshimika zaidi duniani, ambapo hutolewa nchini Marekani kwa wanaofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ya sanaa ulimwenguni.

Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2001 na ‘Black Entertainment Television’, kituo cha runinga kilichopo nchini Marekani.

 

error: Content is protected !!