Namna 4 unavyoweza kutumia maji ya madafu kutunza Nywele zako

HomeElimu

Namna 4 unavyoweza kutumia maji ya madafu kutunza Nywele zako

Ili nywele ziwe na Afya na zikue vizuri zinahitaji kuwa na matunzo, Kuna aina tofauti za utunzaji wa nywele kuanzia uoshaji, utanaji na aina za mafuta ya kutumia kwaajili ya nywele zako. Kuna njia asilia na za kisasa za utunzaji nywele, lakini makala hii hasa itajikita kwenye njia asilia ya kutumia maji ya madafu kutunza nywele kama ifuatavyo.

Maji safi ya madafu
Maji ya dafu husaidia kuongeza unyevunyevu kwenye nywele, ngozi ya kichwa pamoja na kuzipa nywele lishe bora. Ili kupata matokeo chanya unatakiwa utumie maji ya dafu nusu kikombe na uanze kutumia maji hayo kukanda taratibu ngozi yako ya kichwa kwa dakika kama 5 kisha maji ya dafu yaliobaki mwagia nywele zako na uzifunge kwa kitambaa kwa muda wa dakika 20 kisha utaosha nywele zako kwa kutumia sabuni ya nywele (Shampoo) na maji.

Maji ya dafu na asali
Asali inasaidia kulainisha nywele zako kwa kutunza unyevunyevu uliokuwepo kwenye nywele usipotee ili kukupa nywele afya na kuzuia zisiharibike kwa kukatika, Chukua bakuli kisha mimina maji ya dafu robo kikombe na kisha weka asali vijiko 2 vya chakula kisha changanya na upake mchanganyiko huo kwenye nywele kwa muda wa dakika 5 ukianzia kwenye ngozi sugua taratibu na kisha paka kwenye nywele kuelekea juu. Vaa kofia ya kuogea ili kutunza joto au kaa kwenye mvuke kwa dakika 20 kisha unaweza kuziosha nywele zako kwa maji na Shampoo.

Maji ya dafu na juisi ya Aloe vera
Hii ni njia itakupa unyevu kwa muda mrefu zaidi na kukupa afya na inazuia nywele kukatika, Jinsi ya kupata matokeo chanya chukua juisi ya aloe vera, maji ya dafu na mafuta ya mawese kisha osha nywele zako vizuri zikishakauka paka mchanganyiko huo na uziache.

Maji ya limao na maji ya dafu
Juisi ya limao ina vitamini C kwa wingi ambayo inasaidia katika kuzalisha Collagen ambayo inasaidia nywele kukua kwa haraka, unachoptakiwa kufanya ni kuchukua maji ya dafu robo kikombe changanya na juisi ya limao kisha paka mchanganyiko huo kuanzia kwenye ngozi ya kichwa na usugue taratibu mpaka kwenye nywele kote ukimaliza vaa kofia au kaa kwenye mvuke kwa dakika 15 kisha osha nywele zako vizuri kwa shampoo.

error: Content is protected !!