Jifunze mambo 10 ya kipekee kuhusu nchi aliyozuru Rais Samia

HomeMakala

Jifunze mambo 10 ya kipekee kuhusu nchi aliyozuru Rais Samia

Rais Samia Suluhu Hassan yuko nchini Misri kwa ziara ya siku tatu iliyoanza leo (Novemba 10,2021).

Tumekuwekea mambo kumi ya kipekee unayoweza kujifunza kuhusu nchi hiyo iliyopo Kaskazini mwa Afrika.

10. Kalenda ilivumbuliwa Misri

Kalenda yenye siku 365 kwa mwaka ambayo inatumika zaidi duniani, ilivumbuliwa huko Misri.

Historia inaeleza kwamba lengo kuu la kalenda hiyo ilikuwa kutabiri mafuriko yaliyokuwa yakitokea kila mwaka kwenye mto Naili.

9. Vazi la kwanza duniani lilivumbuliwa hapo.

Historia inaonesha vazi la kwanza kuwahi kuonekana ulimwenguni, lilionekana Misri ikiaminika lilivaliwa zaidi ya miaka 5000 iliyopita.

8. Mapiramidi hayakujengwa na watumwa.

Mapiramidi ni kati ya uitambulisho muhimu sana wa Taifa hilo ambapo watu wengi wanaeleza au kufikiri kwamba yalijengwa na watumwa.

Ukweli ni kwamba wajenzi wa mapiramidi waliyajenga na kulipwa ujira, huku ikielezwa kwamba wengi wao walikuwa na na heshima kubwa kwa Farao (mtawala wa Misri ya nyakati hizo).

7. Cairo ndio jiji kubwa zaidi Afrika

Mji wa mkuu wa Misri ni Cairo ambayo inatajwa kuwa jiji kubwa zaidi Afrika na kubwa kuliko jiji lolote katika Mashariki ya kati.

Wakazi wa Cairo peke yake ni zaidi ya milioni 22, ikiwa na eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 500.

6. Watumiaji wa Facebook zaidi ya milioni tano

Misri ni kati ya nchi zenye watumiaji wengi zaidi wa mtandao wa Facebook ambao ni zaidi ya milioni tano huku wakiongezeka kila siku.

5. Mchezo unaopendwa zaidi ni mpira wa miguu.

Mohammed Salah wa Liverpool ya Uingereza, ni mmoja kati wa Wamisri wanaofahamika zaidi ulimwenguni, akiwa mmoja wa wachezaji hodari wa mpira wa miguu kutoka katika nchi hiyo.

Mchezo wa mpira wa miguu unapendwa sana na watu wa Misri, hususan vilabu vya Zamalek na Al Ahly ambavyo vyote hutumia uwanja mmoja (Cairo International Stadium).

4. Hapo zamani, kila mji wa Misri ulikuwa na mungu wake.

Kila mji ulikuwa unaamini katika miungu yake na hivyo Misri ni katika imani tofauti tofauti.

3. Bwawa la Answan ni kati ya mabwawa makubwa zaidi duniani.

Bwawa hilo linakinga maji kutoka mto Naili na kutumika kufua umeme unaotumika nchini Misri.

2. Kiarabu ndio lugha kuu nchini Misri

1. Jua huwaka kwa saa nyingi zaidi.

Answan Misri, ni kati ya maeneo ambalo jua huwaka muda mrefu zaidi ulimwenguni, linaweza kuwaka saa 10 kwa siku.

Kwa mwaka, jua linawaka nchini Misri kwa zaidi ya saa 3451.

error: Content is protected !!