Fahamu upara unaovutia zaidi duniani

HomeKimataifa

Fahamu upara unaovutia zaidi duniani

Mashabiki wa Mwanamfalme William wa Uingereza waliokuwa wanaovutiwa na kipara chake, wafahamu kuwa wanatakiwa kuamisha mapenzi ya kwa nguri wa filamu, Vin Diesel ambaye amechaguliwa kuwa mtu mwenye upara unaovutia zaidi duniani kwa mwaka 2022.

Ushindi wa Diesel (Mark Sinclair) umetokana na utafiti uliofanywa na wakala wa kampuni ua SEO Reboot na kuamua Mwanamfalme wa Whales aondolewe kama mtu mwenye upara mkali zaidi 2022 baada ya muigizaji huyo wa filamu kushika nafasi ya kwanza kwa jumla ya alama 6.46 kati ya 10.

Utafiti huo umeangalia mambo mbalimbali ikiwemo uwiano wa dhahabu usoni (facial Golden Ratio), uchambuzi wa hisia za Twitter, thamani halisi na urefu ili kuamua mshindi.

Kipengele cha kung’aa kwa upara wa kila mshindani pia kilizingatiwa. Vipengele hivi vilitumiwa kuunda alama ya faharasa kati ya 10.

Hatimaye, Diesel alipata alama za juu zaidi kwa takriban vipengele vyote vya faharasa, na kumpa ushindi wa mtu mwenye upara unaovutia zaidi akiwa na urefu wa futi 5.9.

Utafiti huo unaonyesha kuwa kichwa chake kinang’aa na kuakisi mwanga kwa asilimia 70.46 ya mwangaza wa mwanga wa balbu ya kawaida.

Mwigizaji wa Marekani Stanley Tucci aliibuka wa pili kwa alama 6.33, huku mshindi mara mbili Prince William akiibuka wa tano.

Mwigizaji wa “S.W.A.T” Shemar Moore ameingia katika nafasi ya tatu, ingawa ana upara unaong’aa kuliko Diesel, upara wake unaakisi mwanga kwa asilimia 71.85 ya balbu ya kawaida.

Rapa Pitbull amefanikiwa kutinga 10 bora, akitua nafasi ya nne, huku The Rock anayeshikilia rekodi ya mtu mrefu zaidi mwenye kipara katika orodha hiyo akishika nafasi ya tisa.

Mwana wa Mfalme William ndiye mtu wa pili kwa urefu kwenye orodha ya 10 bora, akiwa na futi 6.2, wa pili baada ya Dwayne “The Rock” Johnson, ambaye ana futi 6.4

Hii hapa orodha kamili wa wanaume wenye vipara ambao wamechukuliwa kuwa na mvuto zaidi kuingia kwenye orodha ya 2022:

1. Vin Diesel – 6.46/10

2. Stanley Tucci – 6.33/10

3. Shemar Moore – 6.25/10

4. Pitbull – 6.16/10

5. Prince William – 6.13/10

6. Jason Statham – 5.96/10

7. Bruce Willis – 4.75/10

8. Joe Rogan – 4.37/10

9. Dwayne “Mwamba” Johnson, The Rock – 3.62/10

10. Mike Tyson – 2.50/10

Mwana masumbwi Floyd Mayweather Jr amekosa nafasi ya 10 Bora, akiingia katika nafasi ya 11 kwa alama 2.29.

error: Content is protected !!