1. Shukuru
Kitu cha kwanza kukifanya ukiwa uko kwenye hali ya sitofahamu ni wewe kumshukuru Mungu kwasababu ya hilo gumu. Mshukuru Mungu kwasababu unajua yeye ni mkuu kuliko gumu na kwa maana hiyo muda wa gumu ukiisha utapata furaha yako Ile ambayo imekusudiwa na MUNGU. Kushukuru huwa kuna sababisha nguvu za Mungu zishuke, kwahiyo shukuru tu bila kujali Nani kasababisha wewe kupitia hilo.
2. Omba Moyo wa utulivu
Ukiwa uko unapitia wakati mgumu, fanya kuomba Mungu akupe moyo wa uvumilivu. Uvumilivu ndiyo kila kitu, uvumilivu ndiyo unawapeleka watu kwenye hatima zao. Shetani hataki watu wawe wavumilivu ili wasizifikie hatima zao. Wewe omba ustahimilivu kutoka kwa Mungu bila kujali unapitia gumu gani. Usidharau, wewe omba halafu utaona mabadiliko yalivyo mazuri na makubwa
3. Omba mapenzi ya Mungu yatimie
Kila kitu kinacho tokea huwa Mungu anaona, na Kama ukiwa mtoto wake basi hakuna kitu kitakacho tokea halafu yeye asijue. Huwa anajua unataka uvuke kwenye changamoto Ila yeye Ni humtoa mtu kwenye gumu kulingana na mapenzi yake yanavyotaka. Kwahiyo kuyajua mapenzi ya Mungu hapo itakusaidia wewe kupiga moyo konde zaidi ili usubiri Mungu wako afanye analo ona ni bora kwako
4. Washirikishe watu wenye mitazamo chanya
Jambo lingine la msingi ni wewe kuhakikisha mambo unayo yapitia unawashirikisha watu ambao unajua kwa namna moja au nyingine wanaweza kukusaidia wewe kuvuka, watafute wale ambao hata kwenye nyakati ngumu huwa wako chanya tu, kila wakati wako chanya. Hao watakusaidia kukupa njia za kutatua tatizo lako kwa haraka. Kuna hali fulani ya kujiamini itachipuka ndani yako
5. Soma neno la Mungu
Watu wengi huwa tu wavivu Sana kusoma maandiko kiasi kwamba kuna vitu tunapishana navyo bila kujua halafu huwa ni vya msingi Sana. Neno litakusaidia kujua Mungu anasemaje kuhusu nyakati ngumu, utaweze kujua Mungu huwa anawaokoaje watu wake wakiwa Kwenye changamoto. Elimu hiyo itakusaidia kujua namna unaweza kupambana na Mambo yako ambayo yamekuwa magumu Sa