Gwajima, Polepole kikaangoni

HomeKitaifa

Gwajima, Polepole kikaangoni

Kamati ya Halamashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Taifa imeazimia kuwaita Jerry Silaa, Askofu Josephat Gwajima na Humphrey Polepole ili kuwasikiliza baada ya kujadili taarifa kuhusu mwenendo wao.

Baada ya kuisha kwa mkutano wa kamati kuu ya CCM Taifa chini ya Mwenyekiti wa chama hicho Mhe. Rais Samia Suluhu, kilichofanyika Desemba 17 Ikulu Chamwino mkoani Dodoma taarifa ilitolewa na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka kuwa pamoja na mambo mengine kamti hiyo ilipokea na kujadili taarifa za mwenendo wa wanachama na viongozi wake hao watatu.

“Baada ya kuzingatia kwa kina taarifa hiyo kamati kuu imeazimia kuwaita viongozi hao, ili kuwasikiliza kama inavyoagizwa na kanuni za uongozi na maadil, Toleo la mwaka 2017 na katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2020” alisema Shaka Hamdu.

error: Content is protected !!