Mambo muhimu yakuzingatia kabla, baada ya kununua kondomu

HomeElimu

Mambo muhimu yakuzingatia kabla, baada ya kununua kondomu

Baadhi ya vijana hujiweka katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa yanayo ambukizika kwa kujamiiana bila kutumia kinga kwa sababu manunuzi ya kondomu huambatana na mambo mengi aibu na wengine hushindwa kabisa kununua na kuondoka dukani bila hata kuulizia.

Lakini wataalamu wanashauri ili kujikinga na magonjwa yanayoambukizika wakati wa kujamiiana basi ni vyema wenza wakatumia kondomu ili kuhakikisha kwamba wanakua salama pia kuonana hata na mtaalamu wa afya baada ya tendo.

Endapo wenza wataamua kutumia kondomu, yapo mambo ya kuzingatia kabla, baada na wakati wa kununua bidhaa hiyo,

  • Kitu cha kwanza kujua ni kwamba kununua kondomu ni jambo la kawaida hivyo hupaswi kuona aibu wakati wa kununua.
  • Unashauriwa kununua kondomu zaidi ya paktiki moja ili kukidhi mahitaji wakati wa kujamiiana.
  • Pata muda wa kusoma maelezo muhimu ya kondomu hiyo ikiwemo siku yakuisha muda wa kutumia na malighafi yaliyotengenezewa.
  • Fahamu kama una mzio (allergy) wowote wa kondomu. Zipo kondomu zinazotumia malighafi mbalimbali ikiwemo plastiki, mpira na ngozi za wanyama.
  • Usitumie kondomu ambayo ina dosari yoyote ikiwemo kifungashio kisicho na ubora au maelezo yake hayajitoshelezi.
  • Unapotumia kondomu, soma maelekezo vizuri. Usitumie kimazoea kwani kwani kila siku teknolojia ua utengenezaji wa bidhaa unabadilika.
  • Fahamu mapendeleo yako ikiwemo rangi, fleva ama harufu pamoja na muundo wa kondomu kabla yakununua.
  • Kuwa na uhakika wa ukubwa wa kondomu unayonunua. Zipo kondomu za saizi ya kati, kubwa na ndogo, kwani kununua kondomu kubwa sana au ndogo sana sio salama.
  • Pia unashauriwa kununua kondomu kwenye maduka ambayo utaweza kujichagulia mwenyewe kama utakua unaona aibu mfano maduka makubwa ( supermarkets) na pia kwenye maduka ya dawa ili uweze kushauriwa vizuri na mtoa huduma wa afya.
error: Content is protected !!