Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi imemhukumu Hiari Juma Salumu kifungo cha miaka thelathini jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kujihusisha na biashara ya kuuza bangi nyumbani kwake, kosa ambalo mshtakiwa alikiri.
Polisi wamesema baada ya kupokea taarifa, walifanya upekuzi ndani ya nyumba ya mshtakiwa na kufanikiwa kukamata bangi gramu 56.75.
Mshtakiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani, ambapo alikiri kosa hilo na shauri hilo liliahirishwa hadi Septemba 09,2026 kwa ajili ya kutolewa kwa hukumu.


