Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa ratiba mpya ya vikao vya uteuzi wa watia nia wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani ili kufanikisha mchakato wa kuwapata wagombea.
Hii ni baada ya mabadiliko ya ratiba yaliotangazwa Julai 19, 2025 kupitia kwa Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi Uenezi na Mafunzo ACP Amos Makalla, ambapo alieleza sababu ya mababadiliko ni kuwepo kwa idadi kubwa ya majina ya watiania.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo iliyotangazwa Julai 22, mchakato wa uteuzi utaanza Julai 27 kwa kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa, kitakachofuatiwa na kikao cha Kamati Kuu ya CCM Julai 28, ambacho kitaamua majina ya watia nia wa ubunge na uwakilishi wasiozidi watatu kwa kila jimbo.
????RATIBA YA UTEUZI WA WAGOMBEA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU 2025 pic.twitter.com/dFqaKIrBIN
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) July 23, 2025