Ifahamu ‘CV’ ya January Makamba

HomeMakala

Ifahamu ‘CV’ ya January Makamba

January Yusuph Makamba alizaliwa tarehe 28, Januari, 1974, akiwa mtoto wa kwanza wa Mzee Yusuf Makamba na mkewe Josephine.

Alipata elimu ya msingi huko mkoani Tanga, kabla ya kujiunga na shule ya Galanos (Tanga) na baadae  Forest Hill ya Morogoro. Alikwenda nchini Mrekani na kupata elimu ya juu katika chuo cha St Johns na baadae chuo kikuu cha George Mason alikopata Shahada yake ya Uzamili katika masuala ya Utatuzi wa Migogoro.

Alianza utumishi Serikalini kama Afisa katika Wizara ya Mambo ya Nje, wakati huo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiwa Waziri wizarani hapo. January Makamba aliungana na timu ya Rais Mstaafu Kikwete katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005, na baada ya ‘JK’ kuwa Rais, alimteua January Makamba kuwa Msaidizi wake.

Mwaka 2010, January Makamba aligombea na kuchaguliwa kuwa Mbunge wa jimbo la nyumbani kwako, Bumbuli mkoani Tanga. Katika kipindi cha awamu ya kwanza ya Ubunge wake aliweza kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia (2012-2015)

Mwaka 2015, alikuwa miongoni mwa wanasiasa walioomba ridhaa ya kugombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kwenye kura za maoni aliingia tano bora. Hayati Dkt John Pombe Magufuli ambaye alishinda Urais, alimteua Makamba kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira (2015-2019).

Mwaka 2020, January Makamba alichaguliwa tena kuwa Mbunge wa Bumbuli.

Leo (Septemba, 13, 2021) January Yusuph Makamba ameapishwa kuwa Waziri wa Nishati.

error: Content is protected !!