IMF yaipongeza Tanzania kwa utulivu wa kiuchumi

HomeKimataifa

IMF yaipongeza Tanzania kwa utulivu wa kiuchumi

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Bo Li, ameipongeza Tanzania kuwa na utulivu wa kiuchumi wakati ambao kimataifa mazingira ni magumu.

Amesema hayo wakati akihitimisha ziara yake nchini huku akionyesha azma thabiti ya kusaidia juhudi za nchi katika kufungua uwezo wake wa maendeleo.

“Nimepongeza dhamira ya mamlaka katika kuhifadhi utulivu wa kiuchumi wa Tanzania katika mazingira magumu ya kimataifa,” alisema katika taarifa yake mnamo tarehe 1 Agosti.

“Majibu ya haraka ya mamlaka yamesaidia kudhibiti mfumuko wa bei na kuhakikisha uchumi unalindwa dhidi ya athari za vita nchini Ukraine.”

Bw. Li alizihimiza mamlaka za Tanzania kuongeza uhamasishaji wa mapato ya ndani kupitia marekebisho ya kodi ili kusaidia kuunda nafasi ya kifedha inayohitajika kufadhili matumizi ya kijamii na uwekezaji wa kipaumbele, haswa kuongeza uwekezaji katika rasilimali watu kwa kuongeza matumizi katika elimu na afya.

Ifahamike kwamba, kiwango cha mfumuko wa bei nchini Tanzania kimepungua hadi 3.6% mwezi Juni 2023 kutoka 4.0% mwezi Mei, hivyo kuwa mojawapo ya viwango vya chini vya mfumuko wa bei barani Afrika.

error: Content is protected !!