Jeshi la Polisi kinara vitendo vya Rushwa

HomeKitaifa

Jeshi la Polisi kinara vitendo vya Rushwa

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imezitaja sekta zinazoongoza kwa vitendo vya rushwa nchini huku Jeshi la Polisi likishika nafasi ya kwanza kwa asilimia 45.6 kati ya nne vinara.

Taasisi nyingine ni zile za afya asilimia 17.9, Mahakam ikishika nafasi ya tatu kwa asilimia 11.9 na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) nafasi ya nne, ikiwa na asilimia 6.1 karibu kati yake na sekta ya biashara.

Kutokana na ripoti hiyo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime alisema wanauchukulia utafiti wa TAKUKURU kama moja ya mrejesho wa kuwasaidia kuweka mikakati endelevu zaidi na kuchukua hatua kali dhidi ya askari wenye kuendekeza tamaa binafsi.

“Kujihusisha na vitendo vya rushwa ni kwenda kinyume na sheria za nchi, kanuni za Jeshi la Polisi na miongozo ya dini.

“Tunatoa wito kwa wananchi na wadau wengine tuendelee kushirikiana katika kuzuia na kupiga vita vitendo vya rushwa, kutoa taarifa kwa wanaodai rushwa lakini pia wasiwe chanzo cha kushawishi kutoa rushwa,” alisema Misime.

error: Content is protected !!