Jinsi ya kuwa na uke wenye afya

HomeElimu

Jinsi ya kuwa na uke wenye afya

Uke ni njia ya uzazi, inatupatia raha na pia hedhi kila mwezi hivyo ni lazima uhakikishe unauweka katika hali ya usafi na nadhimu.

Usioshe uke

Watu wengi wamekua wakisikiliza elimu za mitandaoani kuhusu kusafishe uke kwa dawa na bidhaa tofauti, kuwa makina unachotakiwa kusafisha ni eneo la nje tu na sio ndani kwani unaweza ukasababisha magonjwa kutokana na vitu unavyotumia kuoshea.

Shiriki ngono salama

Hakikisha unashiriki ngono salama na una mpenzi mmoja, kwani endapo utakuwa na wenza wengine unaweza kukaribisha magonjwa yanayoweza kukusababishia harufu mbaya ukeni.

Vaa chupi za pamba

Hakikisha pia unavaa chupi zilizotengenezwa na pamba kwani ni malighafi asilia.

Fuatilia afya ya uke wako

Endapo utaanza kuona uchafu usio wa kawaida unatoka ukeni, basi tembelea kituo cha afya, usipuuze.

error: Content is protected !!