Kesi ya Makonda yaondolewa

HomeKitaifa

Kesi ya Makonda yaondolewa

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kinondoni imetupilia mbali na kuiondoa kesi iliyomkabili Paul Makonda juu ya matumizi mabaya ya Ofisi na kuingilia matangazo ya CLOUDS, Hakimu Lyamuya amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Makonda alikuwa akikabiliwa na  mashtaka yaliyofunguliwa na Mwandishi wa habari Saed Kubenea, Katika mashtaka hayo Makonda anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka akiwa mkuu wa mkoa ikiwemo kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds.

MAKONDA KUFIKISHWA MAHAKAMANI

Paul Makonda alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tangu mwaka 2016 alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wakati huo, Hayati Dkt John Pombe Magufuli. Mwaka 2020 Paul Makonda aliondolewa katika nafasi hiyo ikiwa ni baada ya kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kigamboni.

 

error: Content is protected !!