Kijana wa kazi amnyonga bosi wake na kukimbia

HomeKitaifa

Kijana wa kazi amnyonga bosi wake na kukimbia

Kijana wa kazi za nyumbani ambaye jina lake limehifadhiwa anadaiwa kumnyonga kumuua bosi wake kwa kumnyonga kwa kamba ya katani kisha kutokomea. Tukio hilo lilitokea Jumatatu maeneo ya Bombani kata ya Pugu jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Kamishna Msaidizi wa Polisi Moses Fundi amesema inadaiwa mtuhumiwa ni mkazi wa Kaliua mkoani Tabora, Mtuhumiwa alisababisha kifo kwa Cecilia Songomba mwenye umri wa miaka 56 ambaye ni Mkunga mstaafu.

Katika Nyumba hiyo walikua wanaishi watatu marehemu Cecilia, mumewe  na kijana huyo wa kazi za nyumbani, baada ya tukio Mume wa Cecilia anasema siku ya tukio aliporudi nyumbani aligonga mlango bila kufunguliwa ndipo alipoamua kuruka ukuta ili aingie ndani, alipofika ndani alimkuta mkewe amenyongwa kwa kufungiwa chooni akiwa amefungwa kamba ya katani.

error: Content is protected !!