Kikongwe wa miaka 100 mahakamani kwa makosa wakati wa vita ya pili ya Dunia

HomeElimu

Kikongwe wa miaka 100 mahakamani kwa makosa wakati wa vita ya pili ya Dunia

Kikongwe mwenye umri wa miaka 100 ambaye alilitumikia Jeshi la Ujerumani (SS guard) wakati wa vita ya pili ya Dunia, kesi yake itaanza kusikilizwa leo Alhamisi katika nchini Ujerumani.

Kikongwe huyo anashtakiwa kusaidia mauaji ya watu 3,518 wakati akifanya kazi kama mlinzi katika Gereza la Sachsenhausen.  Mtuhumiwa huyo amefanya kazi katika Gereza hilo kati ya 1942 – 1945, ambapo ndani ya kipindi hicho maelfu ya watu walikufa kwa mateso yanayotokana na kulazimishwa kufanya za shuruba, njaa, magonjwa na watu kutumika kama sampuli kwenye tafiti mbalimbali za kisayansi.

Kati ya mwaka 1936 – 1945 zaidi ya watu 200,000 walifungwa kwenye Gereza hili ambalo liko pembezoni mwa mji wa Berlin. Jina la mtuhumiwa bado halijawekwa hadharani, licha ya umri wake lakini atasimama kizimbani kusomewa mashtaka yanayomkabili, ambapo mahakama imetenga siku 22 kwa ajili ya kusoma mashtaka yake.

    > Historia: Mtanzania ashinda Tuzo ya Nobel

Taifa la Ujerumani lipo katika harakati za kuhakikisha kuwa, kila ambaye alichagiza mauaji ya kikatili ya itikadi ya kinazi, basi anafikishwa katika mkono wa sheria kujibu mashtaka.

Fahamu Shida za kawaida na uhasibu kwa wamiliki wa biashara ndogo

Shida na uhasibu kwa biashara ndogo ndogo

Gharama za uhasibu ni sehemu isiyoweza kuepukika ya kufanya biashara, lakini wamiliki wengi wa biashara hutumia pesa nyingi sana kwa gharama za uhasibu kila mwaka.

error: Content is protected !!