Ukiwapata watu hawa 6, unakuwa bilionea

HomeMakala

Ukiwapata watu hawa 6, unakuwa bilionea

Muda huu kuna watu wanatafutwa, ukiwakamata au kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwao, unaweza kuwa bilionea kutokana ahadi zilizotolewa na Serikali ya Marekani.

Wafuatao ni watu 10 wanaotafutwa, na dau lililoahidiwa ukisaidia kupatikana kwao:

6.  Abu Ubaydah al-Anabi

Serikali ya Marekani itatoa dola milioni 7 kwa yeyote atayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa raia wa Algeria, Abu al-Anabi ambaye pia anafahamika kama Yazid Mubarak. Huyu anatuhumiwa kuwa gaidi, akidaiwa kuongoza kundi la al-Qaida na baadae AQIM (Islamic Maghreb).

5. Talal Hamiyah

Huyu ni kiongozi wa ESO (Hizballah’s External Security Organization), kundi ambalo linatajwa kuhusika kwenye kupanga, kuratibu na kutekeleza mashambulizi ya kigaidi nje ya Lebanon, wakilenga zaidi raia wa Israeli na Marekani.

Anasakwa tangu mwaka 2012, atakayefanikisha kukamatwa kwake atapewa dola za Kimarekani milioni 7

4. Salim Jamil Ayyash

Desemba 11,2020, Ayyash akiwa hayupo Mhakamani, Mahakama ilimhukumu kifungo cha maisha, ikisema imejiridhisha kwamba alihusika kwenye shambulio la kigaidi la Februari 2005 huko Lebanon, lililopelekea kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, marehemu Rafik Hariri. Ayyash alidaiwa kuongoza shambulio hilo lililohusisha kujitoa muhanga, ambapo watu zaidi ya 20 walipoteza maisha na wengine  226 kujeruhiwa.

Ukieleza alipo, unapewa dola za Kimarekani milioni 10.

3. Muhammad Abbatay

Anajulikana pia kama Abd-al-Rahman al-Maghreb, ni mkwe wa kiongozi mwandamizi wa kundi la al-Qaida, Ayman al-Zawahiri. Nyaraka ziilizoandikwa kwenye oparesheni ya kumsaka Osama bin Laden mwaka 2011, zilimtaja Abbatary kama nyota anayechipukia katika uongozi wa kundi lao, akisimamia masuala yanayohusu habari.

Marekani inadai kwamba anafanya shughuli zake kutokea Iran, na atakayefanikisha kukamatwa kwake.

2. Muhammad al-Jawlani

Anafahamika pia kama Abu Muhammad al-Golani au a-Jalani. Anadaiwa kuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la al-Nusrah Front (ANF) la nchini Siria. Mwaka 2016 video yake ilisambaa mtandaoni akimsifu kiongozi wa al-Qaida, Ayman Zawahiri.

Mwaka 2015, kundi la ANF chini ya uongozi wa al-Jawlani lilitangaza kwamba limeua watu 20 ikiwa ni baada ya kuteka watu 300 huko Siria.

Ametajwa kushirikiana na makundi mengine ya ugaidi, na atakayefanikisha kukamatwa kwake atapewa dola za Kimarekani milioni 10.

1. Cydey Mizell

Huyu ni mwanamke wa Kimarekani, ana mvi, urefu wake ni sentimita 173 na macho yake ni ya ‘brown’. Yeye sio mhalifu, alitekwa mwaka 2008 huko Kandahar nchini Afghanistan akiwa na dereva wake.

Japokuwa inadhaniwa kwamba watekaji walimuua na kumzika huko Kandahar alikokwenda kufanya kazi kwenye taasisi moja ya kimataifa, Serikali ya Marekani bado haijaondo ahadi yake kwamba atayefanikisha kupatikana kwa Cydey Mizell atapewa dola milioni 5.

 

error: Content is protected !!