Sababu ya Marekani kumzika Osama Bin Laden chini ya bahari.

HomeKimataifa

Sababu ya Marekani kumzika Osama Bin Laden chini ya bahari.

Mei 2, 2011 kikosi maalumu cha Jeshi la Marekani kilimuua Osama Bin Laden, kinara nyuma ya mashambulizi ya tukio la Septemba 11 katika ardhi ya Marekani. Bin Laden kabla ya kukutwa na mauti alikuwa amejificha katika milima ya Abbottabad nchini Pakistan pamoja na wanajeshi wake na baadhi ya wanafamilia kwa karibu.

Jeshi la Marekani baada ya mashambulizi ya mabomu mazito kwenye mlima huo waligundua tayari Osama ameshafariki. Walitekeleza mashambulizi hayo baada ya kupata taarifa za kutosha za kijasusi kuhusu eneo hilo na uwepo wa Osama.

Walipofika walikuta tayari mwili wa Osama umeharibika kwa mashambulizi hayo, waliubeba mwili wake hadi kwenye manuari yao kubwa ya kivita iitwayo USS Carl Vinson hadi bahari ya Kaskazini mwa bahari ya uarabuni na kumzika chini ya bahari siku hiyo hiyo.

Kabla ya kuuzika mwili wake, wataalamu wa masuala ya dini, tamaduni na siasa Marekani waliwaza kwanza namna ya kumzika Osama. Walidhani kwamba kama Osama atazikwa aridhini kama watu wengine, kuna hofu kaburi lake litafanyika kama sehemu ya ibada na matambiko na watu mbalimbali kutokana na ushawishi wake.

Taarifa zinaonesha kwamba Marekani walitaka kumzika Osama Kaskazini Magharibi mwa Pakistan, ambapo katika eneo hilo watu wengi wana imani sana na masuala ya matambiko na ibada za makaburini, wakaona hio haitokuwa sawa kwa siku za mbeleni kwa kuwa ingeumiza hisia za watu wengi duniani na kuleta jazba kwa watu mbalimbali ambapo waliathiriwa moja kwa moja na maisha ya Osama Bin Laden.

Uamuzi ukafikiwa kuchukua mwili wake na kuuzika katika kina cha bahari kuepusha wafuasi wake kufanya kaburi lake eneo la ibada ya matambiko. Kifupi walitaka kufuta kabisa historia yake katika uso wa dunia. Vizazi vitakavyozaliwa mbeleni havitakuwa na uwezo pia wa kuona kaburi lake isipokuwa kusikia tu habari zake.

error: Content is protected !!