Utapeli wa ardhi kwa kutumia mahakama waibuka Dar

HomeKitaifa

Utapeli wa ardhi kwa kutumia mahakama waibuka Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewatahadharisha wananchi kuhusu utapeli mpya wa ardhi unaoendelea mkoani humo kwenye maeneo ya wazi au viwanja ambavyo havina watu.

Makalla amesema watu hao wanatumia ujanja na kutafuta vijana wa mtaani ili kupanga nao njama kuwa wanamiliki ardhi kisha mwisho wa siku wanapelekana mahakamani.

“Wakifika mahakamani yule kijana anakubali kiwanja sio chake. Yule mtu aliyepanga njama anaonekana yeye ndio mwenye kiwanja. “Anashinda kesi halafu baada ya hapo anaanza kufuatilia kuhusu hati mwisho wa yote kunakuwa na double allocation.”

Ametoa angalizo hilo baada ya wananchi mbalimbali kulalamika kuhusu ardhi katika jimbo la Ilala na majimbo mengine aliyofanya ziara.

 

error: Content is protected !!