Matukio 10 makubwa zaidi ya kigaidi duniani

HomeKimataifa

Matukio 10 makubwa zaidi ya kigaidi duniani

 

Katika kuadhimisha tukio la Septemba 11, 2001 lilitokea nchini Marekani miaka 20 iliyopita na kusababisha vifo takribani 3000, ni vyema tukawaleta matukio mengine mabaya zaidi kuwahi kutokea duniani ambayo yamegharimu maisha ya watu.

1. September 11, 2001
Shambulio hili lilitokea nchini Marekani na mpango mashambulizi yalifanywa na kundi la Al – Qaeda. Tukio hilo lilisababisha vifo vya watu takribani 3000, majeruhi zaidi ya 10,000 na hasara ya dola bilioni 10.

2. 2007 Yazidi Communities bombings
Shambulio hilo lilitokea nchini Iraq ambapo watu 2,996 waliuawa kwa mabomu manne ya kujitoa katika eneo la Kahtaniya na mji wa Jazeera, Iraq

3. May 2013 Iraq Attacks
Shambulio hilo lilitokea nchin Iraq na kuuwa watu 500. Tukio hilo lilitekelezwa kwa mfululizo wa kufyatua risasi kwa watu na kulipua mabomu ya kutega katika mikoa ya kati na Kaskazini mwa Iraq.

4. Cinema Rex Fire
Augosti 19, 1978 katika ukumbi wa Cinema eneo la Abadan nchini Iran ulichomwa moto ambapo watu 422 walifariki. Tukio hilo lilitokea wakati wakitazama filamu ya iitwayo ‘The Deer’.

5. Massacre of Trujilo
Tukio hilo ni mfulilizo wa mauaji ya kinyama kati ya mwaka 1988 – 1994 katika mji wa Trujillo Colombia. Watu zaidi ya 400 waliuawa na kikundi cha wahalifu kiitwacho Cali Cartel.

6. July 2013, Iraq Attacks
Llilitokea katika wiki ya kwanza ya Julai 2013, ambapo katika miji tofauti mashambulio yaliyopangwa yaliacha vifo vya watu 389 na kujeruhi wengine 800. Hili lilitokea baada ya vikosi vya jeshi la Iran kuvaamia wapinga serikali katika eneo la Hawija.

7.Beslan School Hostage Crisis
Septemba 1 hadi Septemba 3 zaidi ya watu 1,000 walishikwa mateka kwenye shule ya Belsan nchini Urusi wakiwamo watoto 777. Tukio hilo lilifanywa na watu kutoka nchi ya Chechnia na kundi la Waislamu wa Ingush walioteka shule ya Belsan na kuua watu 385.

8. 2016 Karrada Bombing
Julai 3, 2016 mashambulizi yakupangwa yalitekelezwa Baghdad ambapo watu 341 walifariki na zaidi ya 100 kujeruhiwa. Shambulio hilo lilipangwa kuuwa waislamu jamii ya Shia katika eneo la Karrada ambapo bomu lililotegwa kwenye gari lililipuka na kuua watu wengi ndani ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

9. 2014 Gamboru Ngala Attack
Tukio hilo baya limetoka Mei 5 hadi Mei 6, 2014 katika miji ya Gomboru na Ngala katika jimbo la Bono nchini Nigeria. Watu zaidi 336 waliuawa na kundi la Boko Haram, shambulio hili lilichukua saa 12 kukamilika.

10. Air India Flight 182
Ndege ya biashara ya India kutoka Toronto nchini Canada kwenda Delhi nchini India kupita Montreal na London nchini Uingereza mwaka 1985. Ndege hiyo ilitunguliwa kwa bomu ikiwa futi 31,000 angani na kusababisha vifo vya watu 329.

error: Content is protected !!