Tuzo maarufu za muziki zilizokua zinafanyika nchini Tanzania maarufu kama “Kilimajaro Music Award’’ zinatarajia kuanza kufanyika tena mwaka huu wa 2022, baada ya kuacha kutolewa mara ya mwisho mwaka 2015. Tuzo hizo hutolewa kwaajili ya kutambua mchango wa wanamuziki katika tasnia ya Sanaa.
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema maandalizi yanaendelea na mwisho wa mwezi Machi mwaka huu tuzo hizo zitafanyika, Tuzo hizo zinatarajia kuwa tofauti kwani kuna vipengele vimeongezwa ikiwemo kipengele cha tuzo za kimataifa ambacho kitajumuhisha nchi nyingine zikiwemo Kenya, Nigeria, Afrika kusini na Uganda.
Katika tuzo za mwaka 2015, msanii Diamond Platnumz aliongoza kwa kuchaguliwa vipengele kumi huku akifuatia na Ali kiba ambaye alitajwa kuwania tuzo hizo katika vipengele saba.